Kuhusu sisi

Tanzania Tech ni Tovuti ya Habari na Mafunzo Mbalimbali ya Teknolojia. Tovuti hii ilianzishwa mwaka 2016 hapa Tanzania kwa lengo moja kubwa la kufikisha habari na mafunzo mbalimbali ya teknolojia kwa jamii kwa lugha ya Kiswahili, vile vile tovuti ya Tanzania Tech inasaidia jamii kuelewa kwa ndani kabisa kuhusu teknolojia mpya kutoka ndani na nje ya Tanzania, yote hayo kupitia lugha moja tu ya Kiswahili.

Mpaka sasa tovuti ya Tanzania Tech inawafikia watu mbalimbali kutoka nje na ndani ya mipaka ya Tanzania huku ikifanikiwa kufikisha habari na taarifa zote kwa wana jamii wote waishio kwenye mipaka hiyo. Bado tunaendela kuboresha tovuti yetu pamoja na kuongeza vipengele vipya ili kuhakikisha kuwa hupitwi na habari yoyote ya teknolojia kutoka ndani au nje ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.